NABI KAKIMBIZA DAKIKA 990

Novemba 29,2022 ubao wa Uwanja wa Highland Estate ulisoma Ihefu 2-1 Yanga ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hiyo kupoteza pointi tatu ndani ya ligi wakivunjiwa rekodi ya kucheza mechi 49 za ligi bila kufungwa na kutibua mpango wa kufikisha mechi 50 ndani ya ligi.

Baada ya hapo Yanga imecheza mechi 11 bila kupoteza wala kuambulia sare zaidi ya kushusha vichapo kwa wapinzani ambao walikutana nao.

Ni dakika 990 Nabi kawakimbiza wapinzani wake kwa kusepa na pointi tatu mazima kwenye msako wa pointi 33 kakomba zote.

Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 21 huku ile ya ulinzi ikiokota kambani mabao matatu pekee kwenye mechi za ligi.

Yanga 1-0 Tanzania Prisons, Namungo 0-2 Yanga,Yanga 3-0 Polisi Tanzania,Yanga 3-0 Coastal Union,Azam FC 2-3 Yanga, Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Yanga 1-0 Ihefu, Yanga 1-0 Ruvu Shooting,Yanga 2-0 Namungo,Yanga 1-0 KMC,Yanga 3-1 Geita Gold.