KWENYE mchezo dhidi ya Ihefu mchezaji bora kwa upande wa Simba alikuwa ni Ally Salim na hii inatokana na makosa ya safu ya ulinzi ya Simba yaliyokuwa yakifanywa kila dakika.
Salim ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kayeyusha dakika 90 bila kutunguliwa akiokoa hatari ngumu ikiwa ni dakika ya 5,6,10,15 zote kutoka kwa washambuliaji wa Ihefu wakiongozwa na Yacouba Songne.
Bado Simba licha ya kupata ushindi ina kazi ya kufanyia safu ya ulinzi pamoja na viungo.
Kennedy Juma na Joash Onyango walifanya kazi kwa umakini lakini makosa yalikuwa yakifanyika mara kwa mara kwa upande wao.
Gadiel Michael bado anahitaji kuongeza juhudi kwenye upande wa kupandisha mashambulizi kwa kuwa mapigo yake yote asilimu kubwa yalikuwa yanakwenda nje ya lango.
Ihefu wanapaswa kuangalia upya safu ya ushambuliaji kwenye upande wa umaliziaji.
Nafasi nyingi za dhahabu walitengeneza kipindi cha kwanza Uwanja wa Highland Estate kupitia kwa Adam Adam na Obrey Chirwa ila haikuwa bahati kwao.
Jean Baleke alifunga hesabu jioni kwa kufunga mabao mawili ambayo yameipa pointi tatu Simba.