LIVERPOOL NGOMA NZITO KWA ARSENAL

WAKIWA ndani yà Anfield Liverpool wamekubali kugawana pointi mojamoja na Arsenal ikiwa ni ngoma nzito kwa timu zote kusepa na poiti tatu.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Liverpool 2-2 Arsenal huku kipindi cha kwanza kikiwa ni mali ya Arsenal na kile cha pili wenyeji walifanya kazi kubwa kusaka ushindi nakugotea kuongeza bao moja pekee.

Ni Arsenal walianza kupachika bao dakika ya 8 kupitia Kwa Gabriel Martinell na bao la pili mali ya Gabriel Jesus dakika ya 28.

Liverpool walipachika bao la kwanza kupitia kwa Mohamed Salah dakika ya 42 na kamba ya pili no Roberto Firmino dakika ya 87.

Arsenal inafikisha pointi 73 nafasi ya Kwanza, Liverpool pointi 44 nafasi ya 8.