VIERA ACHAPWA BAADA YA MECHI SABA

PATRICK Viera, Kocha Mkuu wa Crystal Palace alikuwa na wakati mgumu baada ya kunyooshwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ligi Kuu England ikiwa ni baada ya kucheza mechi saba bila kufungwa.

Ilikuwa ni Novemba 27 ambapo alishuhudia Uwanja wa Selhurst Park ukisoma Crystal Palace 1-2 Aston Villa ambayo inanolewa na Steven Gerrad.

Vieira amekuwa kocha bora kuanzia alipojiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu ambapo amefanikiwa kushinda mechi saba mfululizo.

Ni kocha mweusi pekee ndani ya Ligi Kuu England na anawapa tabu wapinzani wake ila ngoma ilikuwa ngumu walipokutana na Aston Villa kwa kuwa hakuwa na ujanja timu yake ilipoteza pointi tatu mazima.

Bao la kufuta machozi kwa upande wake lilifungwa na Marc Gehi dakika ya 90 huku yale ya Aston Villa yalifungwa na Matt Target dakika ya 15 na John Mc Ginn dakika ya 86.