ZAWADI YA PASAKA KUTOLEWA LEO NAMNA HII

ZAWADI ya Pasaka kwa Wanaruagwa inatarajiwa kutolewa saa 3:00 usiku Uwanja wa Majaliwa.

Msako wa pointi tatu kati ya Namungo dhidi ya Mbeya City hatma yake ni zawadi kwa mashabiki wao.

Wakati Namungo ikishuka kusaka pointi tatu dhidi ya Mbeya City itakuwa imeshajua ilichotokea kwa mashabiki wa timu nyingine kipi watakuwa wamepewa.

Ipo wazi kwamba mchezo wa kwanza uliowakutanisha wababe hawa ubao wa Uwanja wa Sokoine ulisoma Mbeya City 2-1 Namungo hivyo leo watakuwa nyumbani Namungo.

Ni Tanzania Prisons dhidi ya Ruvu ambao mzunguko wa kwanza ilikuwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dodoma Jiji hawa itakuwa saa 1:00 usiku dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Coastal Union 0-1 Dodoma Jiji hivyo ni mwendo wa kisasi cha upendo leo.