AZAM FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Mabao ya Issah Ndala dakika ya 39 na lile la pili ni mali ya Idd Suleiman dakika ya 60.
Bao la Mtibwa Sugar dakika ya 75 walikwama kuweka usawa mpaka ilipogota dakika ya 90 kwenye mchezo huo.
Azam FC inafikisha pointi 50 inabaki nafasi ya nne kwenye msimamo nafasi ya tatu ni mali ya Singida Big Stars yenye pointi 51 zote zimecheza mechi 26.