SIMBA YAPIGA HESABU ZA NUSU FAINALI

ROBERTO Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa watacheza vizuri leo dhidi ya wapinzani wao Ihefu.

Simba ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Azam Sports Federation utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru kutokana na matumizi mengie umepelkwa Uwanja wa Azam Complex na ngoma itapigwa saa 1:00 usiku.

Aprili 6 nyota wa Simba walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa leo na miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa katika mazoezi ni pamoja na Clatous Chama, Ismail Sawadogo,Gadiel Michael, John Bocco.

Oliveira amesema:”Tunahitaji kucheza vizuri kwenye mchezo wetu na tunajua utakuwa mgumu tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunahitaji kusonga hatua inayofuata,”.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na Azam FC ambao wao wamepata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar.