TIMU ya taifa ya Argentina inayonolewa na Kocha Mkuu,Lionel Scaloni imeibuka na ushindi wa mabao 7-0 Curacao.
Ni mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Unico Madre de Ciudades.
Katika mchezo huo Lionel Messi ambaye ni nahodha alitupia kambani mabao matatu ilikuwa dakika ya 20,33,37.
Nicolas Gonzalez dakika ya 23,Enzo Fernandez dakika ya 35,Angel Di Maria dakika ya 78 na Gonzalo Montiel dakika ya 87 wakitupia mojamoja.