AZAM FC KUPASHA MISULI NA KMC

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wanatarajia kumenyana na KMC Uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC kesho Machi 27.

Timu hiyo imepoteza vigezo vya kutwaa ubingwa wa ligi baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu na kugotea na pointi zao 47.

Mkononi wana kete tano kukamilisha mzunguko wa pili ambapo hata ikitokea wakashinda mechi zote hawatawafikia pointi vinara Yanga wenye pointi 65.

Kali Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa mechi za kirafiki ambazo wanacheza ni maalumu kwa ajili ya kuwaweka fiti vijana wake kwenye mechi ambazo watacheza kwenye mashindano wanayoshiriki.

“Tunahitaji kuwa imara kwenye mechi ambazo tunacheza tunaamini kuna kitu kitaongezeka kwa wachezaji wetu pale wanapopata muda wa kuonyesha uwezo wao kwa vitendo,” .

Mchezo wao uliopita wa kirafiki Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 JKU ya Zanzibar ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Machi 22.