KMC WAIVUTIA KASI GEITA GOLD

WATOTO wa Kinondoni, KMC wameanza mazoezi kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili 2022/23.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery kituo chake kinachofuata ni dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 11 ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Aprili 17ambapo KMC itakuwa nyumbani.

Miongoni mwa nyota wa KMC ambao wapo tayari kwa mchezo huo ni pamoja na ingizo jipya Hussein Abel ambaye ni kipa aliyekuwa anakipiga ndani ya Tanzania Prisons.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata matokeo.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao na maandalizi yanaendelea chini ya Kocha Mkuu Hitimana mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.