AUBA KAZI HAKUNA TENA

IMERIPOTIWA kuwa Chelsea wapo kwenye mpango wa kuvunja mkataba na staa wao Pierre Emerick Aubameyang mwishoni mwa msimu huu.

Auba amekuwa hana nafasi kikosi cha kwanza ndani ya Chlesea chini ya Kocha Mkuu, Graham Potter.

Tangu ametua hapo msimu huu mambo yanaonekana kuwa magumu kwa staa huyo.

Ilikuwa dakikasaba tu alitumia nyota huyo kwenye mchezo wa Premier ilikuwa Januari 21.

Ripoti zinaeleza kuwa Chelsea inafanya namna ya kumuondoa mwamba huyo kwenye kikosi hicho.

Inaelezwa kuwa Auba hajafanya mawasiliano yoyote na Rais wa Barcelona Joan Laporta ingawa ni matumaini yake kuona anarejea Barcelona huku akipunguziwa mshahara.