DABI YA WANAWAKE KARIAKOO NI MOTO

BAADA ya Desemba 22,2022 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba Queens 1-1 Yanga Princes kesho kazi inatarajiwa kuwa nzito.

Machi 22 kwa mara nyingine tena mchezo wa Dabi ya Kariakoo unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Uhuru.

Unakuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa watani hao kukutana ndani ya Ligi ya Wanawake Tanzania.

Yanga Princess walitangulia kufunga kupitia kwa Wogu Succes na Simba Queens wakaweka usawa kupitia kwa Corozone ambaye alianzia benchi kwenye mchezo huo.