MTIBWA SUGAR YAPOTEZA POINTI TATU MANUNGU

IKIWA kasi ya Simba itaendelea kwa namna hii mpaka kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa angalau ule ubora wa Simba kwenye anga za kimataifa utarejea.

Ubao wa Uwanja wa Manungu umesoma Mtibwa Sugar 0-3 Simba na kaz yote ilimalizwa kipindi cha kwanza kwa mabao ya Jean Baleke.

Mshambuliaji Moses Phiri licha ya kutofunga ametengeneza nafasi nyingi kwa wachezaji wenzake ikiwa ni moja aliyompa Baleke dakika ya tatu kwenye mchezo huo.

Taratibu Clatous Chama na Saido Ntibanzokiza wanaanza kwenda sawa huku Mohamed Hussein akikosa utulivu kwenye mchezo wa leo.

Mtibwa Sugar walikuwa kwenye nafasi ya kufunga dakika ya 71 kupitia kwa Eliuta Mpepo ambapo Air Manula alikoa mpira huo uliompita kwenye mikono yake.

Kipindi cha pili Mtibwa Sugar waliongeza umakini kwenye eneo la ukabaji na kuwazuia Simba kupata bao lingine.