AZAM FC WANAIVUTIA KASI IHEFU

KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kumenyana na Ihefu kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.

Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Kali Ongala tayari wameanza maandalizi kwa ajili ya mchezo huo.

Miongoni mwa wachezaji ambao wameanza maandalizi ni pamoja na Idris Mbombo, Prince Dube, Ayoub Lyanga.

Ongala amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji pointi tatu ugenini.

Itakuwa Uwanja wa Highland Estate, dhidi ya Ihefu saa 10.00 jioni Jumatatu ya Machi 13.