NAMUNGO WAIVUTIA KASI TANZANIA PRISONS

KIKOSI cha Namungo kwa sasa kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo ni wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Machi 11, Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na mazoezi kuikaili Prisons yeye maskani yake Mbeya.

Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja na Shiza Kichuya,Hassan Kabunda, Lukas Kikoti.

Kwenye msimamo Namungo ipo nafasi ya 7 ikiwa imekusanya pointi32 huku Tanzania Prisons ikiwa nafasi ya 14 na pointi zake 22.