UONGOZI wa Singida big Stars umepata dili tamu la kupata udhamini wa kampuni ya uuzaji mafuta nchini inayoitwa NASSCO Limited.
Udhamini huo ni kwa upande wa ujazaji wa mafuta kwenye basi la timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara ikiwa inatumia Uwanja wa Liti kwa mechi zake za nyumbani.
Udhamini huo unaanza kufanya kazi kwenye mechi ambazo zimebaki msimu huu pamoja na kipindi cha msimu mpya wa 2023/24 ambapo basi la timu hiyo litakuwa na uhakika wa kujazwa mafuta kutoka kwa wadhamini hao.
Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars John Kadutu ameweka wazi kuwa jambo hilo ni kubwa na hawatawaangusha wadhamini wao kwenye masuala ya utekelezaji a mpango huo.
“Hili ni jambo nzuri kwa sababu kile ambacho mnakuja kutuwezesha ni jambo kubwa huko nyuma m;ikuwa mnashuhudia kwamba kuna timu zilikwama kufika kituoni kutokana na kukosa mafuta.
“Sasa kama sisi tunapata mafuta je nini kitashindikana utufanya tusifike kituoni na nina amini kwamba kwa namna ambavyo tumeweza kufikia makubaliano haya hakutakuwa na matatizo yoyote kwa upande wa uongozi tutashirikiana vizuri,” amesema.