TUMCHANGIE MDAMU ANAHITAJI MSAADA FAMILIA YA MICHEZO

GERALD Mdamu aliyekuwa nyota wa kikosi cha Polisi Tanzania kwa sasa bado anaendelea kupambana kurejea kwenye ubora baada ya kuumia mguu walipopata ajali ya gari wakitokea mazoezini.

Ilikuwa ni Julai 9,2021 ulimwengu wa mpira ulipatwa ganzi baada ya taarifa ya ajali hiyo ya gari kutokea na mchezaji ambaye alipata maumivu makubwa kuwa Mdamu.

Reagan Senya mtu wa karibu wa Mdamu amesema kuwa muda wa kumtoa vyuma kwenye mguu umefika na ambacho kinahitajika ni fedha jambo ambalo linakwamisha kutokana na hali halisi ambayo ipo.

“Mdamu anaendelea vizuri lakini umefika muda wa kutoa vyuma kwenye mguu wake ambacho kinafanya hayo yasifanikiwe ni kutokana na kukosa fedha ambapo kama tukizipata hata leo atakwenda kupatiwa hiyo huduma.

“Pia tunahitaji kumpata mtaalamu wa masuala ya mifupa kwa kuwa Mdamu bado anafikiria sana kuhusu kurejea uwanjani kucheza jambo ambalo linamkosesha raha kwani ana familia pamoja na watoto ambao wanasoma hivyo akipata mshauri na mtaalamu itakuwa ni faraja kwake,” alisema.

Kwa watakaoguswa kumchangia Mdamu namba ni 0655670101 jina Juliana Malekela.

ReplyForward