ISHU YA UZINDUZI WA JEZI YA KIMATAIFA SIMBA WATAMBA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa uzi mpya ambao wameuzindua leo kwa ajili ya mechi za kimatifa ni bora na utaitangaza Tanzania kwenye anga la kimataifa.

Mtendaji Mkuu wa Simba Iman Kajuna amesema kuwa wanatambua kuwa Tanzania kwenye sekta ya utalii inafanya vizuri hivyo kuongeza nguvu kwenye kuitangaza kutaifanya izidi kufanya vizuri zaizi na zaidi.

“Tanzania ni nyumbani kwa asilimia 50 ya Simba wote duniani, kimantiki hiyo Simba haijakosea kuwa Tanzania. Lakini upande wa pili utalii ndio unachangia pato la fedha za kigeni Tanzania.

“Timu yetu ya wanaume ipo katika timu 10 bora Afrika, timu ya wanawake ni ya nne Afrika na tukiwa na mitandao yenye nguvu Afrika, Tanzania tunaongoza.

“Maana yake tunaweza kutangaza Tanzania na nje ya Tanzania. Simba ikitangaza Tanzania itaongeza pato la Taifa. Jezi za Simba haijavuja,” amesema.

Kwa upande wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano amesema kuwa wamepata baraka kutoka kwa wadhamini wao wakuu kampuni ya M-Bet.

Ni nembo ya Visit Tanzania inabaki kukaa mbele kwenye uzi wa Simba kimataifa.