FEBRUARI 4,2023 itabaki kwenye kumbukumbu za mastaa wa Senegal kutokana na kukutana na kisiki kizito kwenye mchezo wa fainali ya taji la Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani, (CHAN).
Kwenye fainali hiyo dhidi ya Algeria mashabiki walikuwa wanawazomea wachezaji wa Senegal mwanzo mwisho lakini haikuwa bahati kwao.
Dakika zote 120 ziligota kwa timu hizo mbili kutofungana ikiwa ni zile 90 za awali na 30 za nyongeza kusaka mshindi kwenye muda wa kawaida.
Senegal ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti 5-4 ambazo walipata Ageria kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela huko Algeria.
Linakuwa ni taji la kwanza kwa timu hiyo kwenye mashindano hayo.