KWENYE mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Namungo ilipoteza pointi tatu mazima hivyo leo ina kazi nyingine ya kujiuliza mbele ya Yanga.
Aziz KI kiungo mshambuliaji wa Yanga ambaye ni mtaalamu kwenye mapigo huru alikuwa sababu kwenye bao la kwanza lililowavuruga Namungo.
Pigo lake la faulo akiwa nje kidogo ya 18 lilimshinda mlinda mlango Jonathan Nahimana kuokoa likakutana na mtupiaji Yannick Bangala.
Bao la pili ni mali ya mzee wa spidi 120 Tuisila Kisinda likiwa ni bao lake lwa kwanza ndani ya ligi.
Baada ya dakika 90 ilikuwa Namungo 0-2 Yanga, leo kuna kibarua kingine kwa timu hizo kusaka pointi tatu, Uwanja wa Mkapa.
Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo ambao natarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
“Wachezaji wapo tayari na tunatambua utakuwa na ushindani mkubwa lakini ambacho tunahitaji ni pointi tatu,”.