YANGA imetinga hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 70-0 dhidi ya Rhino FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Vijana wa Rhino Rangers wameshuhudia mabao hayo dakika ya 7 kupitia kwa Dickson Ambundo, Kennedy Musonda dakika ya 15, Aziz KI dakika ya 19, Yannick Bangala dakika ya 26 n kiungo Farid Mussa dakika ya 24.
Kipindi cha kwanza ni mabao matano yalifungwa na kipindi cha pili mabao mawili yalifungwa ambapo kipa alifanyiwa mabadiliko Riphat Peter.
Mohamed Ally ambaye alichukua nafasi ya Peter aliokota nyavuni mabao mawili pekee ilikuwa dakika ya 46 kupitia kwa Musonda na dakika ya 90 kupitia kwa David Bryson ambaye alifunga ukurasa wa mabao kwa Rhino.