KMC V NAMUNGO FC KESHO KINAWAKA

“TUNAHITAJI kushinda na sio matokeo mabaya kwenye mechi zetu ambazo tunacheza na kila kitu kinakwenda sawa,” ni Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC.

Timu hiyo inakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Huo ni mzunguko wa pili ambapo kila timu inasaka ushindi kwa hali na mali kufikia malengo yao.

Ni Uwanja wa Uhuru, Januari 24, mchezo huo unatarajiwa kufanyika ambapo timu zote zimefanya maandalizi ya mwisho leo kabla ya kukutana uwanjani.

Miongoni mwa nyota ambao wamefanya maandalizi katika kikosi cha KMC ni pamoja na kipa wao mwili jumba, David Kissu ambaye aliwahi kufanya vizuri kwenye mechi 10 za mwanzo alipokuwa Azam FC.