JEMBE JIPYA ARSENAL KUANZA KAZI LEO

JEMBE jipya ndani ya kikosi cha Arsenal, Leandro Trossard huenda akaanza leo kuonyesha makeke mchezo dhidi ya Manchester United.

Ni miaka minne amesaini ndani ya timu hiyo akitokea Brighton ambayo nayo inashiki Ligi Kuu Engand.

Nyota huyo amesema kuwa ni furaha kujiunga na timu hiyi hivyo atapambana kutimiza majukumu yake kwa umakini akishirikiana na wengine.

Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amesema kuwa anaamini ijana huyo atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.

“Anauzoefu na ligi anajituma na juhudi hivyo nina amini kwamba uwepo wake utakuwa na matokeo mazuri kwetu,” amesema.