MATAJIRI wa Dar, Azam FC hesabu zao kwa sasa ni mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Big Stars, wakulima wa Alizeti.
Timu hiyo imetoka kushinda mchezo wao uliopita na inakutana na Singida Big Stars ambayo nayo imeshinda mchezo wake uliopita.
Singida ilishinda bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar ikiwa ugenini, Uwanja wa Kaitabakwa bao la Bruno Gomes.
Kwa upande wa Azam FC mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Januari 16 ni Ali Ahamada alianza langoni.
Katika mchezo huo dakika 90 zilikamilika ambapo kipa huyo hakutunguliwa bao langoni mwake.
Ubao ulisoma Azam FC 3-0 Tanzania Prisons na timu hiyo ikasepa na pointi tatu kibindoni.
Kituo kinachofuata ni dhidi ya Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Januari 23,2023 Uwanja wa Liti, Singida.
Leo Januari 20 kikosi cha Azam FC kimekwea pipa na Shirika la Ndege Tanzania kuwafuata wapinzani wao.