KIKOSI cha Simba kikiwa nchini Dubai kilicheza mchezo wake wa pili wa kirafiki na kuambulia sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya CSKA Moscow nchini Dubai.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Robert Oliviera Simba iliyeyusha dakika 45 ikiwa imefungwa mabao mawili na wapinzani wao katika mchezo huo.
Kipindi cha pili Simba walionyesha uimara kwenye upande wa kusaka mabao na kupachika mawili kupitia mshambuliaji wao mzawa Habib Kyombo.
Kyombo anakuwa nyota wa kwanza kufunga mbele ya Oliviera kwenye mechi za kirafiki kwa kuwa ule wa kwanza dhidi ya Al Dhafra FC Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Katika mchezo wa jana Kyombo alianzia benchi hivyo kuingia kwake kuliongeza nguvu eneo la ushambuliaji.