MZEE WA KUWAJAZA APEWA MKONO WA ASANTE JANGWANI

HERITIER Makambo amepewa mkono wa asante ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Makambo alirejea ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kusepa kwenda kupata changamoto mpya na Agosti 13,2021 aliweka wazi kuwa ni furaha kwake kurejea ndani ya Yanga.

Makambo amekwama kuwa kwenye ubora wake kutokana na kusumbuliwa na majeraha jambo lililomfanya ashindwe kuwajaza.

Anakuwa mchezaji wa pili kupewa mkono wa asante ndani ya Yanga baada ya Yacouba Songne ambaye naye alikuwa nje kwa muda mrefu.

Yacouba alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting na msimu mzima wa 2021/22 alikuwa nje na msimu huu wa 2022/23 bado alikuwa hajarejea kwenye ubora wake.