NIDHAMU IWE NA MWENDELEZO KWENYE LIGI KUU BARA

MWENDELEZO wa ligi unatarajia kurejea kwa kasi kutokana na kila timu kuwa na shauku ya kupata pointi tatu muhimu.

Huu ni mzunguko wa pili ambao hauna chaguo la nani atafungwa iwe nyumbani ama ugenini mambo yamebadilika sana siku hizi.

Haya yote yanatokana na ushindani uliopo kwani hata zile ambazo zinajiita timu kongwe zimekuwa zikipata ugumu kupata matokeo kwenye mechi za nyumbani.

Iwe hivyo kwenye mechi zote ambazo zinachezwa kwani ligi ya Tanzania ni miongoni mwa zile ambazo zinafuatiliwa kwa ukaribu kutokana na kukua kwake.

Hakuna ambaye anapenda kuona timu yake inashindwa kupata matokeo uwanjani lipo wazi hivyo kurejea kwa ligi iwe ni mwendelezo way ale mazuri ambayo wengi wanatarajia.

Isije ikawa ligi inarudi kisha wachezaji wengi wakaanza kupelekwa kupewa matibabu kwa sababu wameumizwa na wachezaji wenzano uwanjani.

Hili sio sawa mpira una migongano hilo lipo wazi lakini sio kila mchezaji lazima atembeza mikato ya kimyakimya kwa mchezaji mwenzake hata pale isipotakiwa.

Nidhamu kwenye kila mchezo ni muhimu nah ii itawafanya wachezaji kupata matokeo mazuri na timu kupata ushindi bila kuwa na makelele.

Kwa upande wa waamuzi nina amini kwamba wakati huu wa mapumziko mlipata muda kutazama namna ambavyo mlifanya kazi mzunguko wa kwanza.

Kuna kitu kipya kitatambulishwa kutokana na likizo fupi kwa kuwa akili ilipata muda wa kupumzika hivyo mtafuata kanuni na sheria.