SIMBA NDANI YA DUBAI KAMILI KWA KAMBI

KIKOSI cha Simba kimewasili salama Dubai ambapo kitakuwa huko kwa ajili ya kambi ya muda wa siku saba.

Ni Jnuari 7,2023 msafara wa kikosi hicho ulikwea pipa na kuibukia Dubai.

Miongoni mwa msafara huo kulikuwa na benchi la ufundi pamoja na viongozi bila kuwasahau wachezaji ambao wanakkazi ya kusaka ubingwa wa ligi, Kombe la Shirikisho pamoja na kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wana imani kwa namna utulivu wa eneo ambalo watakuwa itawapa nguvu ya kuanza upya.

“Kwa namna ambavyo tunakwenda kwenye eneo la utulivu itakuwa kazi rahisi kwetu kupata nguvu mpya kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu za ligi.

“Tukirudi tutakuwa na kazi dhidi ya Mbeya City tunaamini haitakuwa kazi rahisi ila tutapambana kupata matokeo chanya,”.

Peter Banda, Pape Sakho, Sadio Kanoute, John Bocco, Gadiel Michael, Patrick Rweyemamu ambaye ni meneja wa Simba ni miongoni mwa waliomo kwenye msafara huo.