YANGA KUIKABILI SINGIDA BIG STARS

KIKOSI cha Yanga kesho kina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa pili wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida Big Stars.

Katika mchezo wa kwanza wa mwaka 2023 Yanga ilisepa na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar ambapo dakika 90 zilikuwa ngumu kwa timu zote mpaka muda ule wa lala salama.

Bao la ushindi kwa Yanga ambayo imemtambulisha Muadhathir Yahya kuwa mali yao lilifungwa na Dickson Ambundo dakika ya 90+5.

Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanaamini ushindani utakuwa mkubwa lakini wanahitaji matokeo mazuri.

“Ushindani ni mkubwa na ambaco tunahitaji ni kupata matokeo chanya kwenye mchezo wetu,”