>

AZAM FC KUTUPA KETE YAO KAITABA

KALI Ongala, Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Azam FC inaanza leo mzunguko wa pili baada ya kufunga mzunguko wa kwanza na rekodi ya kushinda mechi 8 mfululizo chini ya Ongala.

Kwenye msako wa pointi 24, Ongala alikomba zote na kuifanya timu hiyo kuwa moja ya timu iliyoweka rekodi yake mzunguko wa kwanza.

Msimamamo unaonyesha kwamba ipo nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 35 inakabiliana na Kagera Sugar iliyo nafasi ya 7 na pointi 21.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi ni pamoja na Idris Mbombo mwenye mabao sita.

Pia yupo Prince Dube, Idd Seleman, ‘Nado’ ambapo jana awalifanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Kaitaba.

 

Ongala amesema:”Maandalizi yapo sawa na morali ipo juu wachezaji nao wapo tayari kwa mchezo wetu,”.