>

MESSI AWATULIZA CROATIA ARGENTINA WAKITINGA FAINALI

NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi amefanikiwa kuandika rekodi nyingine kufika na timu hiyo mara mbili kwenye hatua ya fainali ya Kombe la Dunia.

Ushindi wa mabao 3-0 waliopata mbele ya Croatia kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Lusail Iconic umewapa tiketi hiyo Argentina.

Mastaa wawili muungano wao ulihusika kwenye mabao hayo matatu ikiwa ni yeye mwenyewe Messi pamoja na Julian Alvarez.

Messi alifungua pazia la ufungaji ambapo alipachika bao dakika ya 34 kisha Alvarez alipachika mawili dakika ya 39 na 69.

Sasa Messi atakutana na mshindi kati ya mchezo wa Morroco dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa ambao unatarajiwa kuchezwa leo.

Fainali hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumapili.