SHUKRANI kwa nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye anakuwa ni raia wa Afrika wa kwanza kutoka Afrka kuwatungua Brazil na kuonyeshwa kadi nyekundu wakati akishanglia kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano.
Licha ya ushindi wa bao 1-0 waliopata Cameroon kwenye mchezo wa hatua ya makundi ikiwa ni kutoka kundi G walikwama kutinga hatua ya 16 bora.
Cameroon ilikuwa inahitaji ushindi mbele ya timu ya taifa ya Brazil ambayo tayari ilikuwa imetinga hatua ya 16 bora lakini kikwazo kingie ilikuwa ni matokeo kati ya Uswisi dhidi ya Serbia, jambo lililowapa ugumu Waafrika hao.
Ulimwengu haukuweza kuamini lakini ni matokeo ya mpira, nahodha Aboubhakari alifunga bao dakika ya 90+2 na kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+3 huku mwamuzi akionekana kuwa na furaha kwa kuwa ni sehemu ya mchezo, kuifunga Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia sio kitu chepesi.
Ni kipa namba mbili wa Cameroon, Devis Epassy hakutarajiwa kufanya makubwa kwenye mchezo huo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi kwa kuokoa michomo saba na kuweka lango la Cameroon salama.
Espassy ni chaguo la pili ilibidi awe namba moja baada ya chaguo la kwanza Andre Onana kutibuana na kocha Song ambaye aliamua aondoke kambini nchini Qatar.
Licha ya Brazil kupoteza mchezo huo nyota wao Gabriel Martinell anayekipiga Arsenal alionyesha uwezo mkubwa na timu hiyo inaongoza kundi G ikiwa na pointi sita.
Ilifanya mabadiliko ya wachezaji 8 kwenye mchezo huo jambo ambalo liliwapa nafasi Cameroon kuingia kwa kasi pia nyota wao Neymar Jr hakuwepo kwa kuwa bado anauguza enka.
Cameroon sasa watarejea nyumbani Afrika baada ya kukamilisha mwendo kwenye mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi, Kombe la Dunia Qatar 2022.
Ikumbukwe kwamba Uswisi ilishinda mabao 3-2 dhidi ya Serbia Uwanja wa 974 jambo lililoifanya timu hiyo kufikisha pointi sita ikiwa nafasi ya pili itacheza na Ureno Jumanne kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.