>

RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE YA DUNIA

NYOTA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameweka historia kwa mara nyingine kwa kuiongoza timu hiyo kushinda mbele ya Ghana.

Ghana kutoka Afrika haikuwa na bahati kwenye mchezo uliochezwa Alhamisi baada ya kutunguliwa mabao 3-2.

Nyota huyo alifunga kwenye mchezo huo na aligoma kujibu swali kuhusu kuondoka kwake ndani ya kikosi cha Manchester United.

Ronaldo mwenye miaka 37 aliianza wiki hii kwa kufikia makualiano ya kusitisha mkataba wake ndani ya Old Trafford huku Alhamisi akifanikiwa kuandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano mitano ya Kombe la Dunia.’
Nyota huyo ana ofa ya kutua Al Hilal ya Saud Arabia alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.

“Ni muhimu tumeshinda. Alipoulizwa kuhusu kuondoka Manchester United, Ronaldo alitikisa kichwa na kusema:”Ilikuwa ni wiki iliyomaliza sura nyingine na mguu mzuri, nataka kuisaidia timu yangu na wachezaji wengine wote wa kikosi.

“Huu ni wakati mzuri, nafurahi kucheza michuano hii kwa mara ya tano na najivunia rekodi ya dunia kuwa mchezaji pekee aliyefunga katika michuano mitano ya Kombe la Dunia,”