>

MBEYA CITY 0-1 SIMBA

KITASA wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Simba , Mzamiru Yassin amepachika bao la kuongoza ugenini.

Dakika ya 14 usomaji wa ubao wa Uwanja wa Sokoine ulibadilika na kusoma Mbeya City 0-1 Simba.

Bao la Mzamiru limepachikwa dakika ya 14 kwa pasi ya mshambuliaji John Bocco.

Dakika 45 zimekuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kushambulia kwa kushtukiza.

Nyota ya Sixtus Sabilo mwenye mabao 7 inazidi kuwa kali kwa kuwa ni msumufu kwa mabeki wa Simba.