MASTAA kadhaa wa Yanga leo Novemba 22 wanatarajia kukosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti.
Miongoni mwa nyota hao ni Aziz KI ambaye ni kiungo anayetumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.
Diarra Djigui kipa namba moja wa timu hiyo, Gael Bigirimana kiungo wa timu hiyo hawatakuwa kwenye mpango wa kikosi cha Yanga kwa kuwa walikuwa na majukumu ya taifa.
Pia Heritier Makambo huyu hayupo fiti kwa sasa hivyo atawakosa Dodoma Jiji.
Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu lakini watapambana kupata pointi tatu muhimu.
Yanga imetoka kushinda mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars inakutana na Dodoma Jiji ambayo imetoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya KMC.