MOTO wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala hauzimi kwa kuwashusha waliokuwa namba Simba na sasa wao wapo juu.
Baada ya ubao wa Uwanja wa Majaliwa kusoma Namuongo 0-1 Azam FC, pointi tatu wamesepa nazo jumlajumla.
Inafikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 13 ndani ya ligi kwa msimu wa 2022/23 na Simba wanashuka mpaka nafasi ya pili pointi zao ni 27.
Bao la ushindi limejazwa kimiani na Edward Manyama dakika ya 29 kwa pasi ya kiungo wa kazi Ayou Lyanga.
Kwa upande wa Ihefu ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union umewafanya wafikishe pointi 12 wakiwa nafasi ya 16.
Ni mchezo wa Geita Gold v Mbeya City haukukusanya bao baada ya dakika 90 na wote waligawana pointi mojamoja.