KINARA wa utupiaji mabao ndani ya kikosi cha Azam FC ni Idris Mbombo ambaye ametupia mabao 6.
Bao lake la sita aliwatungua Ruvu Shooting, Uwanja wa Azam FC kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90.
Linakuwa ni bao lake la pili la penalti msimu huu huku likiwa ni bao la kwanza kwake ufunga dakika za lala salama wakati timu hiyo ikisepa na pointi tatu.
Mechi 12 Azam FC imecheza ikiwa nafasi ya kwanza na imekusanya pointi 26 kibindoni chini ya Kaimu Kocha , Kali Ongala.
Ongala ameweka wazi kuwa washambuliaji wake wanazidi kuimarika taratibu licha ya kushindwa kufunga mabao mengi kwenye mechi.
“Wachezaji wanafanya kazi kubwa kwenye kutafuta ushindi na kupata kile ambacho tunastahili, kila mmoja anastahili pongezi ikiwa ni washambuliaji pamoja na mabeki,” .
Ni Sixtus Sabilo huyu ni namba moja kwa utupiaji akiwa ametupia mabao 7 kibindoni.