IHEFU KUMKOSA BEKI WA KAZI KWA MKAPA

TEMMY Felix, Kocha Msaidizi wa Ihefu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuikabili Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara licha ya kumkosa beki wao wa kazi Juma Nyosso.

Ihefu ikiwa imetoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Azam FC inakutana na Simba iliyotoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Singida United.

Ina pointi 5 baada ya kucheza mechi 9 inakutana na Simba yenye pointi 18 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 9.

Felix amesema;”Tunatambua kwamba Simba ni timu bora tunawaheshimu lakini tupo tayari kuikabili kwa kuwa maandalizi yamekamilika.

“Kuna wachezaji ambao tutawakosa ikiwa ni pamoja na Juma Nyosso ambaye ana kadi  nyekundu, Andrew Simchimba, Richard Kinyozi hawa wahatakuwepo lakini wengine wapo tayari,”..