CITY INACHAPA TU, HAALAND ATUPIA

 MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Erling Haaland kwenye mchezo wa Ligi Kuu Enland dhidi ya Fulham alitokea banchi na kufunga bao la ushindi kwa timu hiyo.

Wakiwa pungufu City baada ya nyota wao Joao Cancelo kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 26 ubao wa Etihad ulikuwa unasoma City 1-1 Fulham.

Bao la mapema kwa City lilifungwa na Julian Alvarez ilikuwa dakika ya 16 likasawazishwa kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Andreas Pereira dakika ya 28.

Dakika ya 90+5 Haaland alifunga bao la ushindi kwa mkwaju wa penalti na kufanya ubao kusoma City 2-1 Fulham na pointi tatu zote zikabaki Etihad.

City ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 huku Fulham ikiwa nafasi ya 8 na pointi 19.