AUCHO NA DJUMA KUIWAHI NAMUNGO

KHALID Aucho kiungo msumbufu na mzee wa kazi ndani ya Yanga anatarajiwa kuungana na kikosi leo kwa ajili ya kuelekea Lindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo.

Pia Djuma Shaban naye ambaye ni beki wa kupanda na shaka naye atajiunga na timu hiyo kuwafuata Namungo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na kikosi kitaelekea Lindi leo.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Novemba 20,Uwanja wa Ilulu.

Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 15 wanakwenda kukutana na Namungo iliyo nafasi ya 11 na pointi tano.

Nyota hao walikuwa katika majukumu ya timu zao za taifa katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia ambapo Aucho alikuwa Uganda na Djuma Dr Congo hivyo nyota hao ambao wana uhakika wa namba kikosi cha kwanza watawawahi Namungo.