ISHU YA NABI KUTIMULIWA YANGA IPO HIVI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna mpango wa kumfuta kazi Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kwa kuwa bado wanamtambua kuwa ni kocha wa timu hiyo.

Imekuwa ikielezwa kuwa kwa kushindwa kuipeleka Yanga hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ni sababu ya kocha huyo kuwa kwenye mtego wa kutimuliwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa bado wanamtambua Nabi kuwa ni kocha wa timu hiyo na hawana mpango wa kumfukuza.

“Taarifa ambazo zinasambazwa hizo hazina ukweli kwama tunahitaji kumfukuza Nabi, ambacho kipo ni kwamba yeye bado ni kocha wa Yanga na anaendelea na majukumu yake,” amesema.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga imetolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal hivyo kwa sasa itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Ni dhidi ya Club Africain ya Tunissia Yanga itacheza mchezo wa kwanza ikiazia Uwanja wa Mkapa na ule wa pili itakuwa ugenini kwenye kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Oktoba 23,2022 Nabi anakibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa saa 11 jioni, Uwanja wa Mkapa.