BALAA kwelikweli ndani ya Liverpool ambayo mwendo wake ni mbovu msimu wa 2022/23.
Kocha Jurgen Klopp anazidi kupasua kichwa kutokana na taarifa mbaya kuhusu mshambuliaji wake Luis Diaz kwamba atamkosa mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.
Hayo yote yametokana na maumivu ya goti aliyopata wakati Liverpool ilipoambulia kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Arsenal, Jumapili iliyopita.
Ni pigo kubwa kwa Liverpool, pigo kubwa kwa mashabiki pigo kubwa kwa mchezaji Diaz kuendelea kuipambania afya yake.
Ni mechi 10 mazima nyota huyo atakosekana kabla ya ligi kusimama kupisha Kombe la Dunia lakini ikumbukwe kwamba timu yake ya taifa ya Coluombia ilishindwa kufuzu kama ilivyo Tanzania watakuwa watazamaji tu.