HAALAND NI MWENDO WA REKODI TU

 NYOTA wa Manchester City, Erling Haaland ameendelea kuweka rekodi katika safari yake ya soka akifanikiwa kufunga mabao zaidi ya 20 kwa misimu minne mfululizo.

Haaland ameendelea kuwa tishio ndani ya Premier League msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza kwa nyota huyo kucheza hapo.

Ndani ya Premier League, Haaland amefunga mabao 15, ambapo amefunga katika mechi saba mfululizo alizocheza akiwa na Man City.

Msimu uliopita wa 2021/22 akiwa Borussia Dortmund alifunga mabao 29 katika mechi 30, msimu huu ndani ya City amefunga mabao 20 akicheza mechi 13.