KLOPP AMSHUTUMU KOCHA MKUU ARSENAL

 JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amemshutumu Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta kwa kumpa presha mwamuzi wa mchezo huo Michael Oliver.

Jumapili Arsenal ilifanikiwa kushinda mabao 3-2 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England Uwanja wa Emirates.

Penalti ya staa Bukayo Saka ambayo ilizua utata na ilileta bao la tatu kwa Arsenal ambayo inaongoza ligi.

Ikumbukwe kwamba kabla beki wa Arsenal, Gabriel Magalhaes alishika mpira kwenye eneo la boksi akimzuia Diogo Jota lakini haikutolewa penalti.

Baada ya mchezo huo Klopp amesema hakufurahia kitendo cha Arteta kumpa presha mwamuzi wa mchezo huo.

“Hali ambayo ilijitokeza kwenye penalti nadhani kila mmoja anaweza kukubaliana na mimi kwamba mpira ungepigwa juu mapema, lakini haikuwa hivyo kwani ulirudi tena na ulikuwa mpira rahisi haukustahili penalti.

“Gabriel alishika mpira na mwamuzi akasema kuwa tutazungumzia hilo baada ya mechi kuisha jambo ambalo halikuwa na maana.

“Joe alikuwepo pale na Mikel, (Arteta) nilishangaa akienda kwa mwamuzi, (Oliver) ghafla ikatolewa kadi ya njano tena akiwa mbali,”.