AIR MANULA NA DAKIKA ZAKE BONGO

 

KWA upande wa makipa ambao kazi yao namba moja ni kuzuia mipira kupita kwenye lango lake ni Aishi Manula yeye ni kinara kwa makipa ambao hawajaruhusu kufungwa ndani ya dakika 450.

Akiwa amecheza mechi tano zte za Simba msimu huu wa 2021/22 Manula amekuwa mhimili kwenye upande wa ulinzi na kulifanya lango kuwa salama licha ya timu hiyo kushindwa kushinda mechi zote kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Katika mechi tano ambazo Simba imeshinda huku Manula akitumia dakika zote 450 ni mechi tatu wameshinda na kusepa na pointi tatutatu mazima huku mechi mbili wakigawana pointi mojamoja baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana.

Manula ana clean sheet 5 huku timu yake ikiwa nafasi ya pili na pointi 11 na anafuatiwa kwa ukaribu na Diarra Djigui wa Yanga ambaye huyu ana clean sheet nne na timu yake ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 15.

Mechi za Manula:-Septemba 28, Uwanja wa Karume, Biashara United 0-0 Simba. Oktoba Mosi, Dodoma Jiji 0-1 Simba, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma. Oktoba 27, Simba 1-0 Polisi Tanzania, Uwanja wa Mkapa.Oktoba 31, Simba 0-0 Coastal Union, Uwanja wa Mkapa. Novemba 3, Simba 1-0 Namungo, Uwanja wa Mkapa.

Manula ambaye anapenda kujiita Air Manula ana kibarua cha kutetea taji ya kuwa kipa bora ambayo alisepa nayo msimu wa 2020/21 alicheza mechi 29 kati ya 34 na alikusanya clean sheet 18 ambazo alikuwa nazo.

Pia Manula ambaye ana nafasi ya kucheza timu ya taifa ya Tanzania alikuwa pia kwenye kikosi bora cha msimu uliopita ambapo Simba walikuwa ni mabingwa wa ligi wana kibarua cha kutetea taji hilo kwa mara nyingine tena kwa sasa wakiwa chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco.