YANGA NI WAKALI KWENYE USHAMBULIAJI

YANGA wanaongoza kuwa na safu matata ya ushambuliaji wakiwa wamefunga mabao 9 kwenye mechi nne za ligi huku Simba wakiwa wamefunga mabao 8.

Kwa Yanga ni Fiston Mayele na kwa Simba ni Moses Phiri wanaongoza kwa kufunga mabao mengi ambayo ni matatumatatu, yale ya kufungwa kwa Yanga ni mabao matatu na Simba wamefungwa mabao mawili.

Kwenye mechi mbili za kimataifa ambazo ni dakika 180, Yanga imefunga mabao 9, mchezo wa kwanza ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Zalan na mchezo wa pili ilishinda mabao 5-0 na kufanya isonge mbele kwa ushindi wa mabao 9-0 na safu ya ulinzi haikufungwa.

 Watani zao wa jadi, Simba walishinda kwa jumla ya mabao 4-0, mchezo wa kwanza walishinda mabao 2-0 na ule wa pili mabao 2-0 na kuwafanya wasonge mbele kwa jumla ya mabao 4-0 Big Bullets na safu yao ya ulinzi haikufungwa.