>

KIUNGO WA YANGA AZIZ KI KUIKOSA RUVU SHOOTING

KIUNGO wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia, Stephane Aziz KI anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Nyota huyo hayupo kambini na wachezaji wengine ambao wanajiaandaa na mechi hizo kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Burkina Faso.

Anatarajiwa kuripoti kambini siku ya Jumatatu, Oktoba 3,2022 kutokana na changamoto za Covid 19 aliyoipata akiwa na timu yake ya Taifa.

Aziz Ki alikuwepo kwenye kikosi cha Burkina Faso kilichocheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Comoros uliopigwa Septemba 27, 2022, kwenye Uwanja wa Père Jégo, Jijini Casablanca, Morocco.

Kwa taratibu za afya nchini Morocco wageni hupimwa COVID 19 kila baada ya siku tatu na Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji watatu wa Burkina Faso waliokutwa na maambukizi ya Corona baada ya kipimo hiko kufanyika baada ya mchezo.

Uongozi wa Yanga umefanya jitihada za kuwasiliana na chama cha soka cha Burkina Faso na kupata taarifa kuwa Aziz KI atafanyiwa vipimo vingine na kama mambo yakiwa mazuri atajiandaa na safari ya kurejea Tanzania.