>

WAJELAJELA WASHINDA MBELE YA AZAM FC

AZAM FC imeyeyusha pointi tatu kwa mara ya kwanza msimu wa 2022/23 kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo wa ligi ulichezwa Uwanja wa Sokoine ambapo dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa ngumu kwa timu zote mbili.

Bao la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Jeremia Juma ambaye alitumia pasi ya Ezikiel Mwashilindi aliyetoa pasi hiyo akiwa nje ya 18.

Wajelajela Tanzania Prisons mchezo wao uliopita wa ligi walinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Simba na kuwafanya wapoteze pointi tatu.

Ilikuwa ni dakika za mwanzo kipindi cha kwanza dakika ya 46 bao hilo lilipatikana na kuwafanya Prisons kusepa na pointi tatu mazima.

Ushindi huo unaifanya Prisons kufikisha jumla ya poiti 7 ikiwa nafasi ya 8 huku Azam FC ikiwa nafasi ya sita na pointi zake kibindoni ni 6 zote zimecheza mechi tano.