BEKI MAGUIRE APATA WATETEZI HUKO

NAHODHA wa timu ya Taifa ya England, Harry Kane na beki  Luke Shaw wameibuka na kumtetea mchezaji mwenzao, Harry Maguire.

Beki huyo alifanya makosa mawili yaliyopelekea kufungwa mabao mawili kwenye mchezo uliochezwa Jumatano.

England ililazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Wembley ukiwa ni wa Michuano ya Kimataifa Ulaya.

Maguire alikuwa ni siku nyingine mbaya kazini akifanya makosa mawili dhidi ya Jamal Musiala na kusababisha penalti kabla ya kurejea makosa mengine mbele ya Kai Havertz na kusababishwa wafungwe bao la pili.

Maguire kiwango chake kibaya kimefanya apoteze nafasi kikosi cha kwanza cha Manchester United chini ya Kocha Mkuu, Ten Hag.

Kane amesema:”Ni kweli unapofanya makosa binafsi ni presha na lawama huwa kubwa kwako lakini sisi timu na tunakuwa nyuma ya kila mmoja.

 “Wote watajifunza kutokana na makosa yao na kuendelea mbele wamekuwa watu muhimu kwetu wakati wote na Maguire alipata majeraha ya mguu mwishoni mwa mechi alilazimika kucheza na jeraha ninajivunia ushujaa wake,” .