YANGA YASAINI MIKATABA MIWILI, BILIONI KUKUSANYWA

UONGOZI wa Yanga leo Septemba 12,2022 umeingia makubaliano na GSM kwa kusaini mikataba miwili ya miaka mitano ambayo  itawafanya wavune zaidi ya bilioni 10.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amebainisha kuwa sababu kubwa ya kuinga makubaliano hayo ni utekelezaji wa sera yake ambayo aliingia nayo wakati wa uchaguzi iliyokuwa inalenga kuimarisha nguvu ya uchumi.

Injinia amesema:”Tumeingia mkataba mpya wa kutengeneza jezi na vifaa vya michezo kwa miaka 5 na kampuni ya GSM Group Of Companies wenye thamani ya Tshs Billion 9.1.

“Mkataba huu umefanyiwa maboresho na utakuwa una ongezeko la asilimia 10 kila baada ya mwaka mmoja hivyo ni tija kwa Yanga ukiwa ni mkataba wa kwanza.

“Hii imetokana na faida ambayo GSM wameona hasa kutokana na kuwa na bidhaa bora pamoja na matokeo mazuri ambayo timu inapata.

Mkataba wa pili utakua ni wa udhamini ambapo GSM italipa Tsh. Milioni 300 kwa mwaka, itakayokuwa ikiongezeka kwa asilimia 10 kila mwaka kwa muda wa miaka 5 kuifanya jumla kuwa na Tsh Bilioni 1.83 kwa miaka 5,”.